Friday, July 16, 2010

Masikio; Ngorongoro crater

Kwa kuangalia picha hiii utakubaliana na wadau walioamua kumpa mnyama huyu jina la masikio. wataalam wa tabia za wanyama pori wanasema ya kwamba tembo anapotanua masikio yake kama ilivyo hapo juu si dalili njema. ni ishara ya kukerwa na jambo fulani na huo unaweza kuwa ni mwanzo wa kubadili zoezi. Hutanua masikio yake hivyo ili kumfanya aonekane ni mkumbwa kiumbo kwa lengo la kumtisha adui yake.
Kila mnyama amepewa namna yake ya kipekee ya kuweza kuonyesha hisia/hasira zake pindi anapoona mambo yanaenda tofauti na mpango wake. kujua ishara hizi na kujua nini cha kufanya ndio kuinachomtofautisha mgeni na mwenyeji ktk mambo ya porini. Picha TTB

No comments:

Post a Comment