Friday, July 16, 2010

Kibosho

Ni baadhi ya taswira za safari ya kikosi cha TembeaTz kuelekea Kibosho ambako ndipo geti la kupandia mlima Kilimanjaro kwa kutumia njia ya Umbwe lilipo. Ilikuwa ni siku ya Gulio ktk moja ya vijiji tuilivyopita tukiwa njiani.

Kwenda kibosho unaachana na barabara ya Moshi-Arusha na kuanza safari ambayo ni takriban kilomita 18 hadi kufika geti la Umbwe. Njia panda ipo karibu na eneo lijulikanalo kama msasani/maili sita ktk njia ya Moshi-Arusha

Kama sio mgomba, basi ni buni(kahawa) au mahindi; hali ya hewa nzuri na udongo wa volcano unatoa nafasi kwa mazao mengi kuota na kushamiri vizuri mitaa ya Kibosho

No comments:

Post a Comment