Tuesday, July 6, 2010

alikuwa anatuzuga tusikanyage mayai yake...

wakati nikiwa ktk walking safari toka Maramboi tented camp kuelekea kando kando ya ziwa Manyara tulikutana na huyu ndege ambae alichokifanya awali kilinistaajabisha. Nikiwa ktk Q&A session na guide ghafla tulishtushwa na huyu ndege (Sand Grouse) aliyetua ghafla mbele yetu na kuanza kutuonyesha manjonjo ya ajabu.
Ndege huyu alitua ardhini kama ndege aliyepigwa na jiwe na baada ya kutua akaanza kutanua mabawa yake kama vile ndege aliyejeruhiwa. Kwa haraka haraka nilipata fikra za kwamba ndege huyu atakuwa ni majeruhi. guide alinitonya kwa kusema "hapa tulipo ana kiota chake maeneo haya na lengo lake ni kutupumbaza akili ili tupite mbali na yalipo mayai yake". Hii tabia niliwahi kuisikia, kuiona ktk luninga na kusoma ktk majiradi mbalimbali yanayohusu ndege wa Africa mashiriki an africa kwa ujumla lakini game walk hii ilinipa fursa ya kuiona hii tabia live. Ni tabia ambayo ndege wengi wanaotaga mayai yao ardhini huwa nayo pindi anapohisi uvamizi ktk kiota chake. Hujiangusha chini na kujifanya kajeruhiwa ili mvamizi aachane na mpango wa kutafuta mayai na kisha kwenda kumkamata yeye ambae huwa anakimbilia upande wa mbali na yalipo mayai yake.

Kwakuwa tulikuwa tunakimbizana na muda (jua lilikuwa limeshaanza kuzama) tuliachana na manjonjo ya ndege huyo na kusonga mbele kuelekea kando kando ya ziwa Manyara. Pindi tulipotoka eneo ambalo tulihisi kiota cha ndege huyo kilikuwepo, ndege huyo aliruka na kutokomoea. Ni dhahiri aligundua ya kuwa mayai yake yapo salama na alijua laiti kama angerudi yalipo, tungegundua kiota kilipo. Guide aliniambia hiyo ni tabia yao. Kwani kwa kurudi pale yalipo mayai yake ni sawa na kukuambia kuwa yapo hapa na njoo uyachukue. Kila kiumbe kina namna yake ya kujilinda na kulinda uzao wake.

2 comments:

  1. Nimewahi kuona habari hii ktk documentary kweny national geographic. Pongezi kwako KK kwa kuiona live

    ReplyDelete
  2. DUU HII STORI NIMEWAHI KUIPATA

    ReplyDelete