Wednesday, June 16, 2010

Tulipokutana na Marcio Maximo, Selous GR

katika kipindi alichokaa Tanzania akiifundisha timu yetu ya soka aka Taifa stars, mbrazil Marcio Maximo alikuwa akitumia muda wake wa mapumziko kutembelea hifadhi na mbuga kadhaa ambazo zipo nchini mwetu. Binafsi nilibahatika kukutana na Maximo Sept 2008 ktk pori la akiba la Selous. Awali 'tuligongana' tukiwa ndani ya eneo la hifadhi kama inavyoonekana ktk taswira ya kwanza na baadae tukaonana tena ktk gate la Mtemere wakati wa kutoka ktk hifadhi.

Mimi (shoto) nikila konooz na Maximo. Wakati tupo njiani ku-signout ktk gate la Mtemere tulikutana tena na Maximo nae akiwa njiani kutoka nje ya eneo la hifadhi kurudi ktk campsite aliyokuwa amefikia ktk kijiji cha Mloka, pembezoni kabisa mwa pori la akiba la Selous.

Wadau tuliokuwepo gate la mtemere tulipata fursa ya kupata taswira za ukumbusho na Maximo ambae kwa hivi sasa yupo njiani kurejea kwao Brazil baada ya kumaliza mkataba wake wa kuifundisha soka Taifa Stars. toka shoto ni Said Kasoro, MM, Padre Staphano Kaombe na KK.

Hapa Marcio Maximo alipata wasaha pia wa kupiga picha na baadhi ya wajumbe wa bodi ya shule ya sekondari ya Mt. Anthony Mbagala sambamba na walimu kadhaa waliokuwa ktk safari ya kikazi ndani ya pori la akiba Selous.
Mliosoma St. Anthony secondary miaka ya 90 mnaweza kukumbuka baadhi ya sura za walimu waliofandusha enzi hizo ambao walikuwamo ktk msafara huu. Wazee wa PCM watakuwa wanamkumbuka Mr. Mbungu aliyechuchumaa mbele Mr. Turuka. wa tatu toka shoto (waliosimama) ni Mama Maximo.

2 comments:

  1. hatimae tumeona sura yako mwenyeji,kumbe nakufahamu mdau,poa endelea kusongesha libeneke.

    ReplyDelete
  2. Mimi mwenyewe namfahamu huyu mshikaji, ila sielewagi huo ni mwanya au pengo walikuotea wenye vurugu zao

    ReplyDelete