Wednesday, June 30, 2010

Nilipatwa na uwoga...

Wakati nikiwa na ranger ktk matembezi kwa miguu ndani ya hifadhi ya Tarangire (Game Walking safari) nilikuja kubaina kwamba kulikuwa na kundi la ndege wala mizoga wajulikanao kama Tai likiwa linaruka juu yetu. Kwa uelewa wangu, uwepo wa ndege Tai huashiria kuwa kuna mnyama amekufa eneo hilo na wao wanaendelea kumalizia kile kilichopo, Kwa kawaida, uwepo wao hewani humvutia bwana afya ambae yeye huwatumia kama satelite zake ili kujua wapi kuna msosi wa chee. hali hii huweza kumaanisha kuwa Simba au wanyama wengine wakali wameua mnyama au mnyama kafa kwa namna nyingine za kawaida au kauwawa na majangili. Nilipomuuliza ranger akanihakikishia kuwa hakuna windo lolote lilifanyika eneo hilo kwa kuwa ndege hao wanaruka ktk hali isiyoashiria hivyo.

nilipomuuliza zaidi ni mruko upi unaashirira uwepo wa mnyama kuuwawa au mzoga akaniambia kuwa "Ukiona wanaruka na kushuka chini kwa haraka sana (dive) , basi ujue eneo hilo kuna kitu kisicho cha kawaida". tai tuliowaona walikuwa wanaelea angani bila ya kushuka ardhini hali ambayo ilinipa moyo wa kuzidi kuendelea mbele na walking safari.

Mnapokuwa porini guide(dereva) huwa wanatumia uwepo wa ndege hawa angani ili kujua apeleke wapi wageni kuona aidha Sharubu, wa juu, wa chini au hata bwana afya. lakini sio mara zote hufanikiwa kuwapata hao wanyama.
ranger niliyeambatana nae alinijulisha kuwa hata wao wanapokuwa ktk patrol zao porini, hutumia uwepo wa Tai hewani ili kuweza kujua nini kinaendelea eneo hilo. Kuna siku walifanikiwa kuwakamata majangili ambao walikuwa wameua mnyama na wakawa wapo bize kuchuna ngozi. Wakati wanaendelea na shughuli zao, (majangili) Tai waliwaona na wakaanza kuwazengea kwa kujaa na kuruka hewani huku wengine wakishuka na kutua karibau na eneo uchunaji ulipokuwa unaendelea. Kikosi cha ranger kilichokuwa ktk patrol eneo hilo kilibaini hali isiyo ya kawaida na kusogea karibu. ndipo walipofanikiwa kuwakuta majangili hao wakiwa bize kumalizia kumchuna mnyama waliyemuua isivyo halali ndani ya eneo la hifadhi.

1 comment: