Tembo umuonae upande wa kushoto alivuka barabara na kisha kuvuka mto Tarangire kwenda kumsalimia Tembo umuonae upande wa kulia.
Walipoanza kukaribiana tulianza kudhani pangeweza toke patashika lakini mwisho wa siku tukatanabaisha kuwa hiyo ilikuwa na kama vile sisi binadamu tunapofunga safari kwenda kwa jirani au jamaa aliye mbali nawe kwa lengo la kumjulia hali.
Alipoukunja mguu wake wa kulia (nyuma) ndipo hapo tulipotambua kuwa safari ya tembo huyo ilikuwa ni ya kheri na yenye lengo la kumsabahi mwenzake.
Waliunganisha mikonga yao huko mmoja (aliyevuka barabara na mto) akiukunja mguu wake wa nyuma kulia. Kuunganisha mikonga kwa tembo ni kama vile binadamu tunavyoshikana mikono wakati wa kusalimiana.
No comments:
Post a Comment