Tuesday, June 15, 2010

Hifadhi ya taifa ya Mkomazi

Awali ilijulikana kama Mkomazi Game reserve lakini hivi karibuni serikali iliamua kuipandisha chati kuwa hifadhi ya taifa. Mkomazi National Park inapatikana ndani ya wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro. Ni moja ya hifadhi zilizopo ukanda wa kaskazini wa utalii ambayo umaarufu wake sio mkubwa kama zilivyo Ngorongoro, Serengeti, Manyara, Tarangire n.k.

ni 6 Km toka pale Same unakutana na gate la kuingilia hifadhi ya taifa ya Mkomazi.

Ukiachia kuhifadhi wanyama na mimea mbalimbali, ktk hifadhi hii kuna miradi mikubwa miwili yenye lengo la kunusuru viumbe hai husika kutotoweka. Mkomazi kuna mradi wa kutunza na kuzalisha Mbwa mwitu wakiwa wamehifadhiwa (breeding in captivity). Picha juu ni Mbwa mwitu aka mchakamchaka wakiwa ndani ya eneo wanalohifadhiwa ktk ya hifadhi ya taifa ya Mkomazi. Hapo hutunzwa kwa lengo la kuzaliana na kuongeza idadi ya wanyama hawa ambao inaelezwa ya kwamba wapo hatarini kutoweka.

Sambamba na mchakamchaka, Mkomazi pia kuna mradi wa kuhifadhi kwa lengo la kuongeza idadi ya vifaru. Ahsante ya picha kwa mdau Elly Kimbwereza wa Tona Lodge

No comments:

Post a Comment