Tuesday, June 29, 2010

Game walking safari, Maramboi tented camp

Maramboi tented camp ipo pembezoni mwa ziwa Manyara japo sio ndani ya hifadhi ya taifa ya ziwa manyara. ipo ktk eneo ambalo ni game controlled area. Moja ya mambo ambayo mgeni anaweza kuyafanya akiwa Maramboi ni Game walking safari ambayo inaweza kukufikisha lilipo ziwa Manayara. Nilipojua hii nafasi ipo, sikusita kuomba guide wa kunitembeza na hizi ni baadhi ya taswira chache za matembezi yetu kuelekea Ziwa Manyara toka Maramboi tented camp tulipoweka kambi siku hii. Karibu kabisa na camp kuna bwawa la maji lililojengwa na kusimamiwa na camp. Wanyama huja hapo kunywa maji. Wanyama ambao wanaonekana eneo hili ni Nyumbu, Pundamilia, Aina mbalimbali za swala ikiwemo digidigi, Ngiri. Sambamba na ndege aina mbalimbali ikiwemo Flamingo ambao wao wanapatikana ziwa Manyara.

Hapa ni sawa na kwamba tulikuwa tupo nusu ya safari kuelekea ziwani. majengo unayoyaona kwa mbali ni majengo ya Maramboi camp.

Ni mapito ya wanyama

hapa ni pembezoni kabisa mwa ziwa Manyara. unachokiona ardhini ni magadi yaliachwa kutokana na kina cha ziwa kuendelea kupungua na kukauka. Guide niliyekuwa nae alinidokeza kuwa mwezi February mwaka huu eneo nililosimama wakati napiga picha hii lilikuwa ndani ya ziwa. siku hii ziwa lilikuwa limerudi nyuma mita kadhaa toka hapo. kwa mujibu wa maelezo yake, ziwa Manaara linapungua kina kwa kasi kubwa ambayo inatisha.

Mistari unayoiona ardhini ni alama za miguu ya wanyama waliokuja ziwa Manyara kunywa maji. Mwinuko unaouona kwa mbali ni kingo za bonde la ufa. Ziwa Manyara lipo ndani ya bonde la ufa.

Bofya hapa kupata dondoo zaidi kuhusu Maramboi Tented camp.

No comments:

Post a Comment