Hoteli nyingi zilizopo ukanda wa pwani ya Kunduchi hapa Dar, huwa zinakuwa na huduma ya kupeleka wageni wake kutembelea visiwa vilivyopo sambamba na ukanda huu. visiwa husika ni Mbudya na Bongoyo, japo wengi huwa wanaenda Kisiwa cha Mbudya. Safari huwa zinafanywa kwa kutumia maboti ambayo yanakuwa na injini (out-board engine) pamoja na life jackets kwa kila abiria.
Abiria wakielekea kwenye boat. Kila hotel inakuwa na boat yake na ratiba ya kwenda visiwani na kurudi. Hizi safari namna nzuri sana ya kupumzika kwa weekends. Ukiwa huko ktk visiwa unaweza kutembezwa (kwa miguu) na kujionea mambo mengi ambayo yapo huko, Mibuyu yenye umri wa miaka zaidi ya mia moja. Kuna kaa (crab) ambao wana uwezo wa kunyofoa nazi na kuiangusha chini. kuna viumbe na mimea ambayo huku mjini haipo au ni vigumu kuipata. Kisiwa cha Mbudya kuna pwani nzuri ambayo mkiwa wengi mnaweza kucheza soka, volleyball au mchezo wowote mwingine unaohitaji sehemu ya wazi (na mchanga). Kuna Pwani murua sana yenye mchanga mweupe. Kwa wapenzi wa kuogelea huko ndio kwao, maana hiyo pwani safi sana kwa ajili ya kuogelea.
Kwa taarifa zaidi wasiliana na hotels mojawapo, jangwani see breeze, White sands hotel au Kunduchi beach wakupe mpango mzima.
Niliwahi kutembelea kisiwa cha Mbudya mwaka 2006 na mwaka 2007; Bahati mbaya sana laptop iliyokuwa ni picha za huko ilipata hitalafu ya kiufundi na picha kupotea. Picha hizi za mtundiko wa leo nimezipiga hivi karibuni nikiwa hotel ya White sands.

No comments:
Post a Comment