Ndani ya hifadhi ya taifa ya Lake Manyara kuna eneo lenye maji moto (Hot spring). Sambamba na maji yanayotoka ktk chem chem hiyo kuwa ya moto, pia kuna sulphur ambayo ipo nyingi kiasi cha kuweza kuonekana kirahisi. RAngi ya njano unayoiona ndio sulphur yenyewe hiyo.
Moja ya vivutio vilivyopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Manyara ni Ziwa Manyara lenyewe. Maji ya hili ziwa sio neutral kama yalivyo maji ya mito na maziwa mengine mengi. Ziwa hili huwa na idadi kubwa sana ya ndege aina ya Flamingo ambao wao hushamiri sana ktk maziwa ya namna hii. Flamingo wao chakula chao kikubwa ni algae ambao hushamiri sana ktk maziwa ya namna hii. Ahsante ya picha kwa Mdau AM.
No comments:
Post a Comment