Wednesday, May 12, 2010

Kori Bustard;

Sio kwamba nimeanza kuwatusi wenyeji wangu ni kwamba hilo ndio jina la huyo ndege; Kama kuna aliyeelewa vibaya aniwie radhi. Kama una uelewa wa namna fulani wa ndege wanaopatikana ktk hifadhi zetu hapa Tanzania, unaweza ukamchanganya huyu ndege na ndege mwingine ajulikanae kama Secretary bird. Picha hizi mbili ni za Ndege ajulikanae kama Kori Bustard.

Licha ya kwamba ni ndege na ana uwezo wa kuruka, Kori Bustard hutumia muda wake mwingi wa siku kutembea ardhini ambako ndiko anakopata chakula chake. Hula zaidi wadudu mbalimbali wanaotambaa ardhini. Huwa anaruka pale tu inapobidi. Majike hutaga mayai yao ardhini pia. Hawajengi viota. Picha ya kwanza ni Kori bustard aliyekutwa Ngorongoro na Mdau Thom wa Kima Safaris wakati picha ya pili ni Kori Bustard akiwa ndani ya hifadhi ya Serengeti ambae timu ya TembeaTz ilikutana nae huko.

Kama kuna Mdau mwenye jina la kimatumbi la ndege huyu ruksa kutuhabarisha na kutuelimisha

No comments:

Post a Comment