Friday, May 21, 2010

RADAR ya Wameru dhidi ya Wamasai

Mlima unaounoa ktk picha ya juu upo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Arusha. Kabla ya eneo hili kuwa hifadhi, Mlima huu ulikuwa ukitumika na wakazi wa eneo hili (Wameru) kama mnara wa ulinzi na usalama kwa jamii yao. Wameru walikuwa wakiutumia ili uwasaidie kuona mbali na kuona kama Wafugaji wa Kimasai walikuwa wanaingiza na kuchunga mifugo yao ndani ya eneo lao (Wameru).
Wameru na wamasai wote ni wachungaji. Kutokana na eno hili kuwa ktk eneo lenye rutuba, malisho ya mifugo hupatikana kipindi chote cha mwaka. mambo yakiwa ovyo Umasaini, Wamasai walikuwa wanaingiza mifugo ya na kuilisha ktk maeneo haya yaliyokuwa chini ya umiliki wa kabila la Wameru. Hali ambayo Wameru walikuwa hawakubaliani nayo. Endapo wameru wakifanikiwa kuwaona Wamasai wameingiza mifugo yao, Wameru hupeana ishara na kisha kuchukua tahadhari stahili. Rangi ya mavazi ya kimasai (nyekundu) ilikuwa ikiwasaidia Wameru kuweza kuwaona Wamasai hata wakiwa mbali.
Hii ni moja ya historia ya mila na desturi za jamii zetu hapa Tanzania ambazo nazo zinakuwa zinahifadhiwa ndani ya hifadhi zetu za Taifa. Ahsante ya picha na dondoo kwa Mdau JSK.

1 comment:

  1. Mh, Ya kweli hayo?
    Mila za kimeru kidogo. . . Hapa tupate kuelewa.

    ReplyDelete