Friday, May 21, 2010

Anasubiri hewa ipate joto kiasi ili aruke kirahisi....

Juu ya huo mgunga (acacia) kulikuwa na Tai ambae alikuwa kajikunyata. hawa ndege wa kubwa huwa hapendi kutumia nguvu nyingi kwenye zoezi zima la kuruka. wanatulia mpaka hewa ikipata joto kiasi ndio na yeye aanze kuruka na kupiga misele. ni style ijulikanayo kama soaring kwa kidhungu. Hii haimaanishi ya kwamba usiku hawawezi kuruka, lakini mruko wake muda huo utahitaji nguvu nyingi kuliku mruko huo huo muda wa mchana. Ndio maana ndege wakubwa wa porini ambao huruka (Mtoe mbuni hapo) huwa wanakuwa busy hewani mida ambayo kuna joto la ki ukweli - mchana. Hii ilikuwa ni alfajiri wakati timu ya TembeaTz Ikiwa kwenye Hot air Balloon, Serengeti NP. Picha toka maktaba ya Tembeatz.

No comments:

Post a Comment