Monday, May 24, 2010

Mtemere Airstrip, Selous Game Reserve

Cessna Caravan inayomilikiwa na kampuni ya Coastal Aviation ikiwa inashusha abiria ktk uwanja mdogo wa ndege wa Mtemere - Mtemere Airstrip. Kiwanja hiki kipo ndani ya pori la akiba la Selous karibu kabisa na Kijiji cha Mloka. Ni Moja ya viwanja vinavyotumiwa na makampuni mengi ya ndege kupeleka abiria ktk pori la akiba la Selous. Uwepo wake karibu na kijiji (Mloka) ambacho kina camp nyingi ndio kinachofanya uwanja huu kuwa muhimu kwa hifadhi ya Selous na shughuliza utalii ndani ya Selous kwa ujumla. Coastal Aviation wanafanya safari 2 kila siku (asubuhi na jioni) ktk kiwanja hiki. Selous kuna viwanja vingine ambavyo ni Behobeho, matambwe (zilipo ofisi za Wasimamizi wa hifadhi) na Sand river. Baadhi ya hivi viwanja vya ndege vinamilikiwa na hotel za kitalii zilizopo ndani ya Pori la akiba ili kurahisisha usafiri wa wateja wao. Selous inaelezwa kuwa ni Game reserve kubwa zaidi kwa Africa.
Bofya hapa kujua ratiba za ndege za Costal Avaition kwenda/kurudi Selous na kwenye hifadhi nyinginezo. Picha toka maktaba ya TembeaTz; ilipigwa Oct 2009.

No comments:

Post a Comment