Saturday, April 24, 2010

Wengi huupanda mlima Kilimanjaro kwa malengo mbalimbali

Mdau JSK wa moshi katurushia picha zifuatazo za safari yake ya kuukwea mlima Kilimanjaro kwa kupitia route ya Marangu. Licha ya kwamba kwa 'mwenzie' alikuwa ni moja ya safari zao za adventure, lakini moyoni mwake mdau JSK alikuwa amebeba ujumbe mzito kwa mwenzie. JSK alimuomba 'mwenzake' awe mtarajiwa wake na kwa kuthibitisha aliyoyasema alimvisha pete ya uchumba wakiwa Uhuru point. Ktk tukio hili walikuwa wao wawili sambamba na timu ya wasaidizi (guide + porter) wao.

hapa mdau JSK na mtarajiwa wakiwa wanatembea na kuangalia mandhari mbali mbali zilizoppo ktk kilele cha Kibo peak wakiwa njiani kushuka.

Safari ya kushuka ikiwa imeshika hatamu

Barafu ya Uhuru peak. Mlima Kilimanjaro una 'vilele' viwili ambavyo ndio maarufu zaidi. Mawenzi na Kibo. Kile kilele chenye barafu ndio Kibo, ilihali kile kingine ambacho ni kigumu kupandika ndio kinaitwa Mawenzi. Uhuru Point sehemu iliyo juu kabisa ktk mlima huu ipo ktk kilele cha Kibo.

Mlima Meru ukiwa unaonekana kwa mbali toka Uhuru point. TembeaTz inamshukuru sana mdau JSK kwa kampani anayoitoa kwa TembeaTz kila kukicha. Tunamtakia yeye na mtarajiwa wake kila la kheri ktk mipango na malengo yao. Mungu awabariki na awajalie uwezo wa kupambana na changamoto za maisha
--------------------
Si hasara ukiijua hii.......
Moja ya maeneo ambayo kilele cha Kibo kinaonekana vizuri ni eneo la Kibosho. Neno kibosho linatokana na wakwe zangu waliotangulia kuishi eneo hilo kuunganisha maneno ya
Kibo na Show na kutohoa jina ambalo tumelizoea kwa sasa kama Kibosho.Lilikuwa ni eneo ambali watu walikuwa wanakuja wakitaka kujiliwaza kwa kuangalia kilele cha Kibo.

No comments:

Post a Comment