Tuesday, April 6, 2010

Mbinu za kuhakikisha usalama wa mayai na watoto

Ili kuhakikisha kuwa watoto wao wanakua kufikia hatua ya kujitegemea na wao wenyewe, ndege wengi huwa wana mbinu nyingi za kufikia lengo hili ktk kila hatua ya mchakato huu. Ndege huzaliana kwa kutaga mayai, hivyo jambo la kwanza la msingi ni kuhakikisha kuwa mayai hayo yanatagwa sehemu ambayo hayataharibiwa kwa namna yoyote ile. Ndege ambao mayai yao yana rangi nyeupe, hupendelea kuyaficha ndani ya viota. Wale ambao rangi si nyeupe, huweza kuyatagia na kuyaacha ardhini, japo baadhi yao hujenga viota pia. Kwa Ndege wengi, ni Dume ndie anayejenga kiota ili kumvutia jike kuungana nae. Majike huchagua dume lenye kiota kizuri (kwa viwango vyao wenyewe)

Kwa ndege, sehemu ya kujengea kiota cha kutamia mayai na kisha kulea watoto ni jambo la kuangaliwa kwa makini. Dume huchagua sehemu ambayo haifikiki kirahisi na adui yoyote yule. Utaona ktk picha juu kuwa Ndege huyu amejenga kiota chake ktk Mgunga (Acacia) mti ambao una miiba mikali na kama hiyo haitoshi, tawi la mgunga huu lipo juu ya usawa wa maji - Ziwa Momela dogo. Udogo wa hilo tawi ni kikwazo kingine pia; kiota kinajengwa mwishoni kabisa mwa tawi. Hapo ana uhakika kuwa hakuna atakaeweza kuyafikia mayai au watoto kirahisi na kuleta madhara kwa namna yoyote. Mayai yakitotoa, watoto nao hutunzwa humo humo pia.

Huko Selous, tulikuta yellow weaver bird (msaada wa jina lao kwa kimatumbi) ambao wao hujenga viota vyao ktk matete ambayo yameota pembezoni mwa mto rufiji na kisha matawi ya matete hayo kuelekea ulipo Mto Rufiji.

Yellow Weaver akiwa bize kujenga kiota ili aweza kumvutia bibie kuungana nae na kisha kuanza familia yao. Hii ilikuwa ni ktk mto Rufiji, nje kidogo ya Selous Game reserve, Rufiji. Baada ya hapa, kazi inayofuata ni kulea na kuhakikisha kuwa watoto waliototolewa wanakua bila matatizo na wao kufikia uwezo wa kuwa na miji yao.

2 comments:

  1. BIG Up sana T-E-M-B-E-A Tanzania, post zenu zimeenda shule na zinaelimisha vizuri.
    Endelezi libeneke la kutuhabarisha kuhusu vivutio vyetu na habari nyingine kuhusu maliasili za nchi yetu.

    ReplyDelete
  2. Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi, Yellow Weaver bird ni Ndege Mnana. Katika kushindana kujenga viota vizuri, madume ya ndege hawa hujenga na kukitosa kiota pindi agunduapo kuwa kiota chake hakina mvuto na huendelea hivyo mpaka apate mke!

    ReplyDelete