Monday, April 19, 2010

Maporomoko ya Tululusia - Arusha NP

Wakati wa mapumziko ya Pasaka mwaka huu, Mdau JSK na mtarajiwa wake walifanya safari ya kufurahisha macho na kuliwaza akili ndani ya Arusha National park. Ktk kipindi ambacho walikuwa ndani ya Arusha NP, wawili hawa walifanya game walking safari aka Makanyagio. Safari hii iliwafikisha ktk maporomoko ya Tululusia ambayo yamo ndani ya hifadhi ya Arusha National park. Tululusia ni neno la ki-Meru lenye maana ya sehemu ya kuonea mbali. Maporomoko haya yanaweza kukumbusha Jiografia ya shule ya msingi au hata sekondari.

Ukiangalia kwa makini picha utagundua kuwa kuna tofauti kidogo baina ya miamba iliyopo kushoto na ile iliyopo kulia mwa maporomoko haya. Ukweli ni kwamba, Miamba iliyopo upande wa kulia ni miamba moto (volcanic) na ile iliyopo upande wa kushoto ni miamba tabaka. Mnazikumbuka hizi topic wadau? Ni moja ya vivutio murua vinavyopatikana ndani ya Arusha NP vyenye kuburudisha macho na akili kwa mgeni. Ahsante ya picha kwa mdau JSK wa Moshi.

---------------

Kama mdau ungependa ku-share picha za mandhari nzuri ya nchi yetu (iwe ni mbugani au maeneo ya vijijini) yenye mvuto wa kiasili, unakaribishwa kwa kutuma picha zako kwenye email ifuatayo tembeatz@gmail.com na maelezo mazuri ya picha utakazotuma nasi tutaziweka hewani.

KK

No comments:

Post a Comment