Mchaka mchaka ni jina la porini walilopewa mbwa mwitu. jina hili wamepewa kutokana na tabia yao ya kukimbia -ku troti - muda mwingi. Hutumia muda mwingi kukimbia na kupumzika muda mchache. Maisha yao ni ktk kundi na hata uwindaji wao ni wa uvamizi. kundi moja linaweza kuwa na mbwa mwitu kumi na kuendelea. Tofauti na simba, mbwa mwitu wao huanza kumla mnyama waliemwangusha hata kabla hajafa. Simba, Chui na wengine huhakikisha kwamba mnyama amekufa na ndio hapo wataanza kumla. Mchaka mchaka hawana huu ustaarabu.
Hivi sasa inaelezwa ya kwamba wanyama hawa wapo ktk hatihati ya kutoweka, ndio maana juhudi kadhaa za kuwanusuru zinafanyika ili waendelee kuwepo. Picha juu ni kituo kilichopo ndani ya Mkomazi National Park, Same ambako hawa jamaa wanatunzwa kwa lengo la kuzaliana ili kuweza kuongeza idadi yao - breeding in captivity. wakizaliana vya kutosha hurudishwa porini ili kuendelea na maisha kama kawa.

NI KITU GANI KINAFANYA HAWA WANYAMA WAWE KWENYE HATIHATI YA KUPOTEA NAOMBA JIBU MDAU NINA HAMU SANA YA KUJUA MAANA SIPATI LOGIK
ReplyDelete