

licha ya kutoa punguzo la viingilio, kuna haja kubwa ya kuwa na nguvu za pamoja ili kuweza kuongeza idadi ya Watanzania wanaotembelea hifadhi mbali mbali zilizopo nchini. Swala hili lina marefu na mapana yake, TANAPA wamejitahidi kwa uwezo wao. Changamoto inabaki kwetu wadau wengine ili kutimiza azma ya Utalii wa ndani. Utalii wa ndani ukipanda, uwezekano wa kuondokana na msimu wa utalii (High na Low season) upo. mwaka mzima ukawa ni msimu wa utalii. Njia mojawapo ya kutimiza azma ya kupeleka watanzania wengi ktk hifadhi na mbuga zetu ni kwa kufanya safari za makundi ili kuweza kupunguza gharama mbali mbali za safari za porini. hili si jambo geni kwani hata 'watalii wenyewe' wengu huja kwa makundi ili kupunguza gharama kwa upande wao.
No comments:
Post a Comment