




Kuna tofauti kubwa sana kati ya mtu kukaa ndani au nje ya Hifadhi. Unapokaa ktk hoteli iliyo nje ya Hifadhi (karibu na mipaka wa hifadhi), kwa kiasi kikubwa mazingira yake yatakuwa hayatofautiani sana na yale ya nyumbani kwako ulikokuacha. Sambamba na hii, unakuwa upo mbali na wanyama ambao umesafiri kilometa nyingi kuja kuwaona na kuwafurahia.
Unapoamua kutembelea mbuga au hifadhi, jaribu kufanya mpango walau usiku mmoja upate kulala ktk hotel iliyopo ndani ya Hifadhi. kama una moyo (kama kikosi cha Tembea) fanya tented Camping ktk camping sites au la kama roho nyepesi basi lala ktk hotel ya kawaida.
Unapoamua kutembelea mbuga au hifadhi, jaribu kufanya mpango walau usiku mmoja upate kulala ktk hotel iliyopo ndani ya Hifadhi. kama una moyo (kama kikosi cha Tembea) fanya tented Camping ktk camping sites au la kama roho nyepesi basi lala ktk hotel ya kawaida.
Unapolala ndani ya hifadhi, moja ya vitu vitakavyokusisimua (ukibahatika), ni milio ya wanyama mbalimbali ambayo utakuwa ukiisikia mida ya usiku. Hii ni hali ya kawaida usiku kwani sauti huwa inasafiri umbali mrefu usiku kushinda mchana.
Hapo utaweza kumsikia bwana Afya (fisi) akiwa kwenye mishemishe zake za kuzengea mawindo ya wenzie au mizoga waliyoiacha. kama ukiwa karibu na mto au bwawa basi Viboko nao utawasikia bila wasi wasi, masikio (Tembo) nao utawasikia wakitoa milio yao mida ya usiku. Na hata Sharubu pia kwa mbali au hata kwa karibu. Sambamba na milio ya wanyama wakubwa, milio ya ndege mbalimbali nayo huwa haikosekani.
Milio hii ya wanyama sio kitu ambacho tumekizoea ktk maisha yeti ya kila siku hali ambayo itakupa msisimko wa kipekee na kuifanya safari yako ya porini kudumu akilini mwako muda mrefu na kukufanya utake kurudi porini tena na tena.
Wengi huingia porini kwa lengo la kuona wanyama, lakini kuna mengi mengineyo ya kujifunza kuhusu wanyama na mazingira yao. na baadhi ya haya mambo unapata fursa ya kujifunza na kuyajua pindi unapokuwa karibu na wanyama ktk vipindi tofauti tofauti (Usiku na mchana).
Ndani ya Hifadhi ya Ruaha kuna sehemu nyingi za malazi, Ruaha river lodge ni mojawapo. kama unapenda camping basi kuna camping sites kadhaa baadhi nyingne zikiwa kando kando ya mto ruaha. tented camping ni njia mojawapo ya kukusogeza karibu kabisa na wanyama. ktk yote haya hakikisha unayafanya ukiwa na guide mwenye uelewa au wewe mwenye uwe na uelewa mkubwa na mambo ya porini na wanyama pori.
No comments:
Post a Comment