Picha mbili za juu nilizipiga nikiwa juu ya hicho kilima kinachopatikana maeneo ya Area D.
Kilima hicho kinaitwa Simba hill
Kuna siku wakati wa kipindi cha somo la Jiografia, mwalimu aliniuliza nitaje maeneo ndani ya Tanzania ambayo ni jangwa. Moja ya neno nililotoa kama jibu langu lilikuwa ni Dodoma. Na mwalimu akasema nimepata. kwa bahati mbaya sana dhana hii ilijengeka kichwani mpaka nilipotembelea Dodoma mwanzoni mwa mwaka 2008 (kwa mara ya kwanza) na kuikuta Dodoma sio jangwa kama nilivyodhania hapo awali.
Picha juu ni moja ya maeneo ambayo yanilinafanya nipingane kwa namna fulani na dhana ya kwamba Dodoma ni Jangwa. wenye lugha yao wanasema a picture says a thousands words, ni dhahiri Dodoma si jangwa kama wengi tulivyodhania wakati tunasoma shule za Halmashauri.
No comments:
Post a Comment