Thursday, December 31, 2009

Njia ya Songea - Iringa

Milima maarufu ya Lukumburu inayofahamika na kuheshimika na madereva wa njia hiyo kwa kona zake kali na za hatari. ukiwa unasafiri kutoka Njombe kwenda Songea dereva lazima uwe makini sana na hizi kona. cha msingi ni kuhakikisha unakaa ktk site yako muda wote - hasa hasa kwenye kona.

Hapa ni kipande cha kutoka Njombe kuelekea Makambako. ni ile sehemu yenye mashamba ya Chai pande zote za barabara. Mashamba hayo yapo nyuma ya miti unayoiona pembezoni mwa barabara.

Stendi ya Treni ya TAZARA ya Makambako, ni stendi muhimu sana kwa wafanya biashara ya mbao toka mkoa wa Iringa. Bidhaa kuu inayosafirishwa toka hapo ni mbao toka ktk misitu iliyopo maeneo kadhaa mkoani Iringa.

Misitu inayotoa mbao ya Mafinga

No comments:

Post a Comment