Monday, November 30, 2009

Tembea ujionee maajabu

nguzo zikiwa upande wa kushoto mwa barabara ukiwa unatokea Makambako.

Nyaya za umeme zikahamia upande wa kulia (nguzo ya pili mbele utaona nyaya zinahamia upande wa kulia wa Barabara)
makaburi chini ya mti, nyaya zikiwa upande wa Kulia wa barabara
------------------------------------------

Ukiwa unasafiri kutoka Makambako kuja Iringa mjini, utapita eneo linaloitwa Tanangozi. Moja ya mambo ambayo hustaajabisha wengi wanaosafiri ktk barabara hii ni kuhama ghafla kwa nguzo za umeme (I'm sure ni za Tanesco) toka upande mmoja wa barabara na kurudi upande wake wa awali ktk umbali mfupi tu!

Niliwahi sikia hizi habari lakini hivi majuzi nilipata bahati ya kujionea mwenyewe hali hii. Mengi yanaweza kusemwa lakini kikubwa kinachoelezewa ni kwamba;
Nyaya za Umeme zilipopita juu ya makaburi , umeme ukawa hauwezi kupita- nikimanisha toka kule unapotoka hadi kueleka kule unapotakiwa kwenda destination.
baada ya mafundi kuhangaika sana wakagundua kuwa umeme 'unapotea' nguzo moja kabla ya nyaya zao kupita juu ya hayo makaburi. Baada ya majadiliano na consultation, timu ilikubaliana kuwa ili kuweza kukamilisha kazi, nyaya hizo zivushwe upande wa pili wa barabara ili zisipite juu ya makaburi na kuwezesha umeme kupita kama inavyotakikana. na mita kadhaa baada ya makaburi, nyaya zikarudishwa upande wake wa awali wa barabara ili kuweza kuendelea na safari.

Tembea uone...

1 comment:

  1. Duh!
    Hii kali! lakini mbona makaburi ya Ubungo yahasumbui kiivo!? Na nyaya za umeme zimepita juu?
    Duh!

    ReplyDelete