Wapo wanaomjua kama Drogba huku wengine wakimfahamu kama Mwananyika. Ni mdau wa Utalii ukanda wa Selous (Mloka) ambako yeye hujishughulisha na shughuli ya kusindikiza wageni kwenye safari za Matembezi maeneo ya pembezoni ya pori la akiba la Selous huko Mloka, Rufiji. Safari hii nae alielekea ukanda wa kaskazini na kuwakilisha utalii wa kanda ya Kusini kama anavyoonekana kwenye picha hizi.
Jina la Drogba amepewa sababu ya sura yake kuonekana kufanana na ya Mwafrika mwenzetu anayesakata kabumbu huko bara la Ulaya, Didier Drogba. Mwenyewe hupenda zaidi kutumia jina la Mwananyika, jina ambalo hulitaja pia kwenye nyimbo zake anazoziimba akiwa kwenye misafara yake na wageni kwenye mapori ya kijiji cha Mloka. Safari zake hujaa mafundisho mengi na mazuri kuhusu mahusiano baina ya wanyama pori, wanadamu na mazingira ambayo sote tunatumia pamoja.
Picha Arnold Ulomi - Road to Africa
No comments:
Post a Comment