Tuesday, June 16, 2015

Boat Safari ndani ya Mto Rufiji, Selous Game Reserve

Selous Game Reserve Tanzania Boat Safari Rufiji River
Moja ya mambo ambayo huwa vinanifanya niwashauri watu waende Selous badala ya Mikumi (kwa wale wa Dar) ni wingi wa mambo ambayo mgeni anaweza kuyafanya akilitembelea pori hilo. Sio tu Game Drive lakini pia Safari za Boti huku ukiangalia na kuona wanyama waliomo mtoni na hata waliopo pembezoni mwa mto Rufuji. Ni safari zenye raha ya kipekee ndani ya mto Rufiji.

Selous Game Reserve Tanzania Boat Safari Rufiji River
Mgeni anaweza kufanya boat safari ndani ya eneo la hifadhi au nje ya hifadhi. Kwa safari za ndani ya Hifadhi nyingi husimamiwa na kambi za wageni zilizopo ndani ya hifadhi, pembezoni mwa mto Rufiji. vivyo hivyo kwa nje ya hifadhi, Hoteli zilizopo pembezoni ya Mto huwa na boti na wasaidizi kwa ajili ya boat safari kwenye mto rufiji. Gharama hupishana, ndani ya hifadhi kukiwa na gharama zaidi ya nje ya hifadhi. japo kwa safari za Ndani ya pori, mgeni anakuwa na nafasi kubwa ya kuona baadhi ya wanyama wakubwa na adimu. kwa huku nje zaidi ni Ndege, Mamba, viboko na wanyama jamii ya swala.

Selous Game Reserve Tanzania Boat Safari Rufiji River

Selous Game Reserve Tanzania Boat Safari Rufiji River

Selous Game Reserve Tanzania Boat Safari Rufiji River
Jua linazama kwa mbali. Boat Safari inaweza fanywa muda wowote kulingana na ratiba ya mgeni. Asubuhi, mchana au hata mida ya jioni kabla ya jua kuzama.

Selous Game Reserve Tanzania Boat Safari Rufiji River

Selous Game Reserve Tanzania Boat Safari Rufiji River
picha zote kwa hisani ya Mdau Arnold Ulomi wa Road 2 Africa

No comments:

Post a Comment