Thursday, January 1, 2015

Heri ya Mwaka mpya 2015

Napenda kuchukua fursa hii kwanza kabisa kwa Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa Neema na Rehema zake kutuwezesha kuufikia mwaka huu mpya wa 2015. Ni zawadi adhimu aliyotujaalia ili tuweze kumtumikia kwa namna mbalimbali. 
Blog yenu ya Tembea Tanzania inapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru nyote mliokuwa nayo sambamba kwa mwaka 2014 ktk jitihada za kuhabarishana na kuhamasishana khs dhana ya Utalii kwa Watanzania almaarufu kama Utalii wa Ndani. Timu ya Tembea Tanzania inapata faraja kubwa kuona idadi ya Watanzania wanaoamua kwenda maeneo mbalimbali ya utalii kwa mapumziko kipindi hiki cha mwisho wa mwaka. ni Ishara ya kwamba dhana ya Utalii kwa Watanzania inaanza kupata msisimko na kushika kasi nzuri. Ni safari ndefu lakini kwa mwelekeo huu unaoendelea ni dalili kuwa tunaelekea vyema. Tunawapongeza wale wote walioenda hifadhi za taifa mbalimbali na maeneo mengine ya Utalii ndani ya Tanzania yetu.

Ni matumaini yetu kuwa mwaka 2015 utakuwa na ongezeko la idadi ya wazalendo wanaoelekea kwenye pwani, Mapori na Milima ya Tanzania kwa mapumziko yao. Kuijua Tanzania na maeneo yake ni hatua nzuri ya kujenga UZALENDO kwa taifa letu.

Heri ya Mwaka Mpya 2015.

KK for Teambea Tanzania Team.

1 comment:

  1. Heri ya Mwaka Mpya TembeaTz Team.
    Huwa siachi kutembelea hapa angalau mara moja kwa wiki kama nimebanwa sana.
    Keep it up KK. Tupo pamoja
    Mdau Michael

    ReplyDelete