Monday, December 8, 2014

Simba Public Campsite, Ngorongoro Crater

Ni Picha zenye kuonyesha mandhari mwanana ya Campsite ijulikanayo kama Simba Campsite huko Ngorongoro crater. Campsite hii ipo nje ya crater, pembezoni ya barabara inayozunguka crater na ile inayoelekea Serengeti NP. Licha ya kuwa nje ya crater, campsite hii hupata kutembelewa na wenyeji (nikimaanisha wanyama pori) wa eneo hili kama inavyoonekana kwenye picha ya juu ambapo Pundamilia kadhaa wamesogea karibu na mahema ya wageni. Ngorongoro crater aka Shimoni ndio inayoonekana kwa nyuma kwenye picha ya juu.


Ngorongoro crater ina aina ya uhifadhi ya kipekee sana. ni Eneo la uhifadhi ambalo wanyama pori na wanadamu wameruhusiwa kuwa pamoja. Japo picha hizi zinabeba mandhari ya utalii, lakini sio jamba la ajabu kukuta vijana wa kimasai wakiwa wanachunga mifugo yao ndani ya Crater sambamba na wanyama wengine wa porini.

Ni muonekano wa hali halisi ya campsite. Simba campsite ni public campsite. Kwa kuitwa public Campsite inamaanisha hapa wageni wanakuwa wanaishi pamoja kwenye eneo moja. mgeni anayelipie gharama, hupewa ruhusa ya kujenga hema lake na kujihifadhi kwa muda anaotaka. Ukiachana na public campsite unakutana na private campsite ambapo mgeni au kampuni moja ikifanya booking basi wageni wengine hawataruhusiwa kuweka mahema yao eneo hilo. gharama kati ya hizi mbili hutofautiana pia.

Matukio kama haya mimi hupenda kuyaelezea kama wenyeji wanakuja kuwasalimu wageni wao. Kwa kusema hivi namaanisha wenyeji wanyama pori na wageni ni sisi ambao tunaenda kuwatembelea. Hii ni kwenye Simba campsite ambapo Tembo hawa walikuja kunywa maji kwenye matenki ya kuhifadhia maji kwa ajili ya wageni.



wapo waliotaharuki na kushika kilicho chao tayari kwa kuchukua mwelekeo wowote wa kujihamoi.

shukran ya picha hizi kwa Mdau Rajab wa Wildness Safaris Tanzania

No comments:

Post a Comment