Tuesday, December 9, 2014

Maandalizi ya Safari ya Diving - Nungwi, Zanzibar

Zanzibar Diving
Hivi karibuni nilipata fursa ya kujaribu kitu kipya nilipokuwa kisiwani Unguja kwa mapumziko mafupi ya mwisho wa wiki. Ni moja ya mambo yalikuwa kwenye list ya vitu vya kujaribu walau mara moja na kisha kuamua kuendelea nacho au kuachana nacho. Ilikuwa ni kufanya safari fupi ya Diving (kupiga mbizi) na nilipata fusra hii kwenye Hotel ya La Gemma Del Est huko Nungwi, Zanzibar (Unguja). Diving ni jambo la hatari na hivyo kabla ya safari lazima mgeni apewe elimu ya kutosha kuhusu mambo muhimu ya kufanya unapofanya diving. Maandalizi huanza kwa kuangalia Video yenye kuelezea mambo kadha wa kadha kuhusu diving ambayo huchukua takriban dakik 45. 

Zanzibar Diving
Baada ya hapo Mgeni hukutanishwa na Mkufunzi wake - kwa safari yangu mimi alikuwa ni Bw. Haji Kushoto kwenye picha juu - ambae hutuoa maelekezo ya ziada na ufafanuzi wa vifaa muhimu. Mnapomaliza maelekezo hufuatia maandaliza ya diving gears ambapo mkufunzi humpa fursa mgeni kuandaa vifaa vyake chini ya usimamizi wake wa karibu. 


Zanzibar Diving
Hatua ifuatayo baada ya hapo ni kwenda kufanya jaribio la kuogelea na vifaa vya diving kwenye bwawa la kougelea au eneo la kina kifupi baharini. Kwa siku hii tulienda kufanya jaribio hili kwenye ufukwe wa kina kifupi. Hii ina lengo la kumwezesha mgeni kumudu vifaa mbalimbali anavyokuwa amevivaa na stamina yake. Jaribio hili linaweza kumpeleka instructor na diver mpaka eneo lenye urefu wa Mita nne chini ya usawa wa bahari. Mawasiliano baina ya mgeni na Instructor ni jambo ambalo linajaribiwa kwa umakini na ufasha sana. Ieleweke ya kwamba, kwa diving za namna hii mawasiliano baina ya wazamiaji ni kwa njia ya alama za mikono tu. Bofya hapa kuzielewa vyema alama hizo.

Zanzibar Diving
Mtungi wa gesi sambamba na miguu ya bata inaweza kukupa changamoto kwenye hatua za awali lakini ukifanya mazoezi madogo unaweza kupata control na kuyamudu kwa muda mfupi tu. Boya la rangi ya chungwa aliloshika Mkufunzi ni kwa ajili ya kuelea juu na kuwezesha wengine kufahamu kuwa hapo chini kuna watu wanapiga mbizi. Kwa safari hii ya jaribio, tulienda umbali wa Mita 3.5 chini ya usawa wa juu wa bahari. Kimsingi niliweza kukumbana na changamoto kadhaa ambazo zilinifanya niweza kutumia maelekezo niliyopewa kabla ya safari; Maumivu kwenye sikio kadri unavyozama chini na jinsi ya kukabiliana nayo ili uweze kuendelea mbele. Maji kuingia kwenye kioo chako na jinsi ya kuweza kuyatoa ukiwa ndani ya maji na kadhalika.

Zanzibar Diving
Jambo jingine la muhimu ambalo mgeni hujifunza ni kuhusu kupumua kwa kutumia mtungi wa gesi. Ni jambo la rahisi lakini linahitaji majaribio ili kuweza kulimudu vyema. Safari hizi za majaribio zinalenga pia kumwezesha instructor kujua matumizi ya gesi ya mtungi ya mgeni wake. Wapo watu ambao hupumua kwa haraka na hivyo kumaliza hewa yao mapema mno na wapo ambao hupumua taratibu na hivyo kudumu kwa muda mrefu na gesi wanayozama nayo chini. Kiwango cha upumuaji kinasabibishwa na mambo mengi ikiwemo ukubwa wa mwili/kifua cha mtu au tabia ya uvutaji wa Sigara. Kitu cha msingi ni kwamba ni jambo la hatari kwa mtu aliye na mafua kufanya diving. hii inaweza leta maumivu makali kwenye masikio na hata madhara kama hatositisha zoez.

Zanzibar Diving

Zanzibar Diving
Moja ya vutu ambavyo diver huvaa ni kifaa kinachoweza kujazwa upepo na kumwezesha diver kuelea juu ya maji bila shida, endapo atataka kuzama basi anakuwa anbofya mahali na kutoa upepo na kisha yeye ataanza kuzama chini. Hapa niliweza kuelea kwa kumsaada wa kifaa hicho ambacho huitwa Buoyancy Control Device (BCD).

Zanzibar Diving
Baada ya maandalizi haya, ndipo tulipofanya safari yetu ya kina kirefu kidogo mbali na nchi kavu. huko tulienda umbali wa karibu mita saba chini ya usawa wa bahari. Licha ya kuwa na kina kifupi, tuliweza kuona mengi ambao yalinipa hamasa ya kuweza kuitamani na kuisubiri safari ya kina kirefu kwa hamu. Kwa mujibu wa Guide wangu alinidokeza kuwa wapo wageni ambao huamua kuishia na safari hiyo na kugeuza kwa sababu mbalimbali binafsi, nyingi zikiwa ni uoga. Nilifanikiwa kuweza kumudu uzito wa mtungi wa gesi mgongoni na kuweza kuji-balance na kuogelea vyema. Uogeleaji wa diver ni tofauti na uogeleaji wa kawaida kwani kwenye diving mikono haitumiki sana - inakuwa huru. Miguu (ikisaidiwa na ile miguu ya bata) ndio inafanya kazi kubwa ya kumwezesha diver kusonga mbele. Mikono inabaki kuwa na kazi ya mawasiliano na kushika nyenzo nyingine muhimu - ikibidi.

1 comment: