Tuesday, September 23, 2014

Sharubu wa Tarangire

Mdau Abdul Kimanga, CEO wa Respect DJs na mdau mwandamizi wa ShereheYetu.com alikuwa kwenye mapumziko mafupi huko Tarangire na hizi ni baadhi ya picha alizoweza ku-share nasi. Hili kundi la Sharubu lilikuwa limepumzika kivuli kabla ya Swala mmoja kukatiza karibu yao na wao kuanza mishemishe ya kutaka kumkamata na kumfanya kitoweo. Swala huyo aliweza kuwachomoka na kuwaacha midomo wazi kama ambavyo mdau Abdul alivyoweza kuwanasa na camera yake.
Shukran ya Picha kwa Mdau Abdul Kimanga wa www.shereheyetu.com 

No comments:

Post a Comment