Mikindani ipo nje kidogo ya Mji wa Mtwara. Ni moja ya miji mikongwe na yenye umuhimu wa kihistoria kwa taifa letu. Ni mji ambao ulijengwa wafanyabiashara wa Kiarabu. Historia inaonyesha mji huu ulijengwa mnano karne ya Tisa. Wajerumani na Waingereza (Wakoloni) walipata kuutumia mji wa Mikindani kama moja ya vituo vyao vya utawala kwa ukanda wa Kusini.
Pwani hii ipo pembezoni kabisa ya barabara kuu inayounganisha mji wa Mtwara na mikoa ya Lindi na Dar es Salaam. Kama utaingia Mtwara kwa gari ukitokea Dar au Lindi basi ni dhahiri utakatisha maeneo haya unapoingia Mtwara. Mikindani ipo takribani kilometa kumi tokea Mtwara Mjini.
Pwani tulivu yenye madhari nzuri.
No comments:
Post a Comment