Wednesday, September 17, 2014

misele ya hapa na pale ndani ya Mtwara

 Tulipata wasaha wa kuzungushwa kidogo na wenyeji wetu ili tujionee maeneo kadhaa ya mji wa Mtwara na Viunga vyake. Picha hizi zina lengo la kukupa taswira ya hali ilivyo ki miundombinu. Hizi zimepigwa maeneo ya nje kidogo ya mji wa Mtwara.Mitaa mingi sasa hivi imewekewa Lami kama inavyoonekana kwenye picha hizi huku ujenzi ukiendelea kwenye baadhi ya maeneo muhimu.


Eneo hili lipo karibu na bandari ambapo shughuli za ujenzi zinaendelea

Matenki yanayotumika kuhifadhi mafuta.

Mtambo wa zamani wa kuzalishia umeme kwa njia ya Diesel ambao sasa hivi hautumiki tena. Mji wa Mtwara na maeneo ya jirani yanapata umeme unaozalishwa kwa njia ya Gesi. 

Maeneo ya pembezoni mwa Bandari ya Mtwara. Bahari na Bandari vipo upande wa Kulia.

Kwa sisi tunaoishi Dar, barabara hii ya Mtwara naweza kuifananisha na Mandela Road kwa hapa Jijini Dar. Ni barabara kuu inayoiunganisha Bandari na maeneo mengineyo. kule mtwara inajulikana kama Bandari road.

Meli ikionekana kwa mbali ikiwa gatini kwenye bandari ya Mtwara. 

No comments:

Post a Comment