Monday, March 17, 2014

Drogba wa Mloka - Selous Game Reserve

Mwananyika aka Drogba wa kule mloka akitoa maelezo ya awali kwa wageni wake kabla hawajaanza safari ya matembezi kwa miguu kwenye mapori na vichaka vilivyopo pembezoni ya pori la akiba la Selous, kwenye kijiji cha Mloka huko Rufiji. Yeye huzungusha wageni wanaotaka kujifunza zaidi kuhusu wanyama, na safari na zake huwa ni kwa makanyagio - walking. Safari hizi huchukua muda wa zaidi ya saa moja ambapo wageni wanaweza kukutana na wanyama kwa karibu japo hizo nazo hutegemeana na upatikanaji wa wanyama kwenye maeneo ya nje ya pori. Wageni wa Drogba hupata kujifunza mengi kuhusu tabia za wanyama pori, mazingira yao na mahusiano ya wanyama hao na wanajamii wa vijiji vilivyopo kando kando ya pori la Selous. Hapa ni kwenye camp ya Hippo.akitoa pozi ndani ya moja ya mapori akiwa na wageni wake

Picha zote kwa hisani ya Mdau Kanuth Tarimo wa Kanuth Adventure safaris

No comments:

Post a Comment