Thursday, February 20, 2014

Selous Game Reserve leo mchana (20th Feb)

Sharubu hawa bibi na bwana walikutwa na Mdau Thomas wa HSK Safaris mida ya leo mchana ndani ya Pori la akiba la Selous. Walikuwa eneo lijulikanalo kama Mbuyu wa Nyuki karibu kabisa na ziwa la Nzelekela. Nidhahiri Sharubu hawa walikuwa Valentine maana walikuwa wawili tu na mara nyingi wanapojitenga na kwenda faragha namna hii, huwa ni kwa malengo ya kuongeza idadi ya familia yao. Njia anayoifuata sio njia ya kupita watu, ni njia iliyotengenezwa na wanyama wanaopita hapo kwenda Ziwani kunywa maji. Baada ya kuwa Harusini kwa siku kadhaa, njaa imeanza kuwasumbua na wanaanza kutafuta mkao wa mawindo ili waweze kupata chochote kuwatuliza njaa yao.Sharubu jike alikuwa katulia tuli huku Dume likiwa linarandaranda eneo hilo
Unapokuwa porini na kukuta sehemu ina michoro mingi ya matairi kama unavyoona kwenye hii barabara, basi ujue hiyo si sehemu ya kuipita kwa kasi. Kuna jambo zuri la kuliangalia kwa makini. Mara nyingi huwa ni uwepo wa wanyama adimu ambao wengi huangaika kuwapata ili wawaone. Huu ni uthibitisho mwingine kuwa Sharubu hawa walikuwa eneo hilo kwa muda mrefu kwani matairi ni mengi yakielekea kila upande. Ishara kama hizi hutumika sana na guides wanapokuwa porini ili kuweza kufanikisha sightings za wanyama adimu.

Kwakuwa Selous ni pori la akiba (Game Reserve), Off Road driving inaruhusiwa, ndio maana baadhi ya matairi yametoka mpaka nje ya barabara. Kwenye hifadhi za Taifa hili ni kosa linaloweza kukupelekea kutozwa adhabu ya $400 endapo askari wa wanyama pori watakukamata na kukutia hatiani. Epuka Off Road driving uendeshapo ndani ya hifadhi ya Taifa hata kama umefika ene lenye mnyama adimu uliyehangaika kumtafuta siku nzima.


Shukran ya Picha kwa Mdau Thomas wa HSK Safaris aliyepo huko Selous kikazi.

No comments:

Post a Comment