Sunday, February 2, 2014

Linganisha upate kubaini ukubwa wa Simba aka Sharubu

Sharubu ndani ya Ngorongoro Crater aka Shimoni. Ni picha aliyonitumia mdau Assery hivi karibuni ikimuonyesha Sharubu jike akiwa amekaribia kabisa gari ya wageni "wake". Napenda uingalie na kuweza kulinganisha na kubaini jinsi hawa jamaa walivyokuwa na mauombo makubwa. Ni maumba haya na misuli yao ndio inayowawezesha wakawinda na kuuwa mnyama mkubwa kama Nyati, Tandala (Kudu) au hata Twiga ambao wamewazidi maumbo. Wakati mwingine wapo ndugu zetu ambao hudiriki kumlinganisha Simba na Mbwa, labda akiwa mdogo lakini simba mwenye umri wa miaka zaidi ya minne huwa na umbo kubwa la kumchachafya mwanadamu bila kufurukuta. Shukran kwa mdau Assery wa Arusha kwa picha hii.

No comments:

Post a Comment