Sunday, February 2, 2014

Horombo Hut, Marangu Route - Mount Kilimanjaro

Hii ni hali ya kituo cha Horombo kwenye siku ambayo ni ya jua kali. Kwa hapa Juu hali inakuwa ya jua lakini ukanda wa chini unaweza ukawa na mawingu na hata mvua kubwa kama inavyoonekana kwenye picha hii. Siku hii maeneo ya uwanda wa chini yalipata mvua za kutosha wakati huku juu kulikuwa na jua zuri tu.Safari ya kupanda mlima Kilimanjaro inakupa fursa ya kuyaona mawingu yakiwa chini yako huku wewe ukiwa umesimama kwa miguu yako mwenyewe ardhini - sio kwenye ndege.


Baadae Jua liliachia na walio maeneo ya chini wakapata mwanga wa jua

 Bandaz za kulala wageni. Njia ya Marangu ndio njia pekee ya kupandia Mlima Kilimanjaro ambayo ina mabanda ya kulala wageni. Njia nyingine zote wageni wanalala kwenye mahema yao wanayobeba wenyewe

 Mashamba ya miwa ya TPC Moshi yakionekana kwa mbali kutokea kituo cha Horombo mida ya Jioni

 Kilele cha Mawenzi kinakuwa kipo kwa nyuma tu ya kituo cha Horombo - japo ni mbali ki mwendoKilele cha Kibo nacho kinaonekana vyema pale hali ya hewa inaporuhusu.
picha zote ni kutoka maktaba ya TembeaTz

No comments:

Post a Comment