Tukijiandaa kuanza safari ya matembezi kwa miguu (Game Walking Safari) ndani ya pori la akiba la Selous. Hapa ilikuwa ni kwenye geti la Mtemere. Unapofanya safari hizi ni lazima muambatane na Askari wa wanyama pori ambaye anabeba Silaha. Hii ni kwa ajili ya kutoa ulinzi kwa wageni. Mlinganyo unaotumika ni kwamba Askari mmoja huangalia wageni wasiozidi watano. Kama mtakuwa wageni kumi basi mtalazimika kuwa na askari wawili. Sambamba na Askari pia mnakuwa mnaambatana na msindikizaji (Guide) ambaye jukumu lake kubwa ni kutoa maelezo mbalimbali ya wanyamapori na mazingira yao. Kushoto Ni Ranger (mwenye silaha) na kulia ni guide tuliyeambatana nae. Mimi ni wa pili kushoto na aliye kushoto kwangu ni Ndugu yangu niliyeambatana nae - Bavon
Vitu vingine unaweza ukavipuuzia unapokuwa kwenye gari lakini unapofanya walking safari hata kinyesi cha tembo huwa ni topic ya kufundishwa muwapo safarini. mita chache baada ya kuanza safari yetu tulikutana na lundo unaloliona ambapo guide wetu alitueleza mambo kadha wa kadha kuhusu kinyesi cha Tembo.
Moja ya jambo lilinogusa ni kuhusu sababu ya Kinyesi cha Tembo kutumika kama dawa ya magonjwa na matatizo mengi ktk Jamii mbalimbali za kiafrika. Sababu kubwa inayochangia Imani hiyo inatokana na Ukweli wa kwamba Tembo hachagui chakula. Kuanzia mimea midogo midogo mpaka magome ya baadhi ya miti. Mfumo wake wa mmeng'enyo wa chakula sio mzuri sana hali ambayo hufanya kile kinachoingia kwenye Tumbo lake kutoka kikiwa kama hakijasagwa vyema. Ni mchanganyiko huu wa miti na majani mbalimbali, sambamba na udhaifu wa Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula kunakopelekea kinyesi cha Tembo kuonekana ni kama mkusanyiko wa miti shamba mbalimbali. Uwepo wa Miti ya aina nyingi ndio kunakopelekea Kinyesi cha Tembo kutumika kama dawa kutibu magonjwa mbalimbali kwenye jamii nyingi za kiafrika hususan zile zinazoishi kwenye maeneo wanakopatikana Tembo aka Masikio.
Hii ni njia ya viboko wanapotoka na kurudi mtoni.
Pango la kujificha mnyama lililotelekezwa.
Picha hii niliipiga kwa lengo la kuonyesha utofauti uliopo kwenye ulaji wa vyakula kwa wanyama mbalimbali. Hili ni tunda ambalo linatoka kwenye miti ya mikoche - palm trees. Tunda halisi ni hilo la upande wa Juu kulia (Jekundu). hayo mawili na mabaki ya tunda hilohilo lakini kila mmoja lilikuwa limeliwa na mnyama tofauti. La chini lilishambuliwa na Nyani/Ndegere wakati la juu kushoto liliwa na Tembo.
Njia nyingine ya viboko na wanyama wengine kuelekea kwenye mto Rufiji
huu ndio ukaribu unaoweza kuupata kuwa na wanyama wa porini. Twiga ni waoga sana na mara chache watakuruhusu uwasogelee karibu. Hawa walitustahi sana, japo sekunde kadhaa baadae walianza kutimua mbio na kutokomea porini.
Ni mtu unaotumiwa na tembo kujikunia wadudu wanaowakwaza.
Tukiwa tumetokomea ndani ya pori la akiba la Selous kwa Miguu. hapo tukiwa tumefika eneo ambalo tulikubaliana kugeuza na kurudi Geti la Mtemere. Tulitembea kwa miguu takribani saa moja huku tukiweka vituo vya hapa na pale kwa lengo la kupata maelezo na dondoo mbalimbali.
Alikufa kwenye mapigano na boko wenzake lakini wahifadhi wakakusanya mifupa yake na kuipanga kwa lengo la kuwaelimisha wageni kuhusu mfumo wa mifupa wa kiboko.
Uwanja wa Ndege wa Mtemere.
Wenyeji wakisubiri wageni wao wafike na ndege. Wageni ambao husafiri kwa ndege hupokelewa na magari ya wenyeji wao na kisha kuendelea na ratiba zao. Mara nyingi huwa ni magari ya hoteli wanazofikia au makampuni ya Tours ambayo huandaa magari ya kuwapokea.
Picha zote toka kwenye maktaba ya TembeaTz
mh, sounds scary, mgekutana na carnivores wa aina yeyote ile protocol yao inakuaje sasa?
ReplyDelete