Sunday, October 27, 2013

Wanaitwa Mchakamchaka kwa ile lugha ya Porini

Ukiwa porini na ukasikia neno mchakamchaka linatajwa basi ujue hapo ni Mbwa mwitu ndio anasakwa. Wamepewa jina hili kutokana na tabia yao kuwa wanakimbia kwa muda mwingi wa siku yao. Hupumzika muda mchache na kuendelea na mizunguko yao. Majuzi Mdau Thomas wa HSK safaris aliwafuma ndani ya pori la akiba la Selous huko Rufiji. Walikuwa wamepumzika kwenye kivuli.

No comments:

Post a Comment