Thursday, October 17, 2013

Mzee wa Kazi (Simba aka Sharubu) alikuwepo hapa... Saadani


Saadani National Park
Hatukubahatika kumuona mwenyewe lakini tuliona nyayo zake, Tulielezwa ya kuwa siku iliyopita eneo hili kundi moja la Sharubu liliua mnyama na kushinda hapa siku nzima. Waliofanya game drive siku hiyo walipata fursa ya kuwaona sharubu hao ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani. Hifadhi ya Saadani ina Simba japo uonekanaji wao ni mgumu kidogo tofauti na hifadhi nyinginezo.Saadani National Park

Saadani National Park
Pembeni ya eneo lililokuwa na nyayo za Simba kulikuwa na Ngiri ambaye alikuwa akiendelea kula Nyasi bila wasiwasi. Uwepo wake na hali ya utulivu aliyokuwa nayo Ngiri huyu ilidhihirisha ya kuwa Wakuu wa kazi walikuwa wameshasepa eneo hili na kuhamia eneo jinge kuweka mtego wa windo jingine la mlo.

No comments:

Post a Comment