Monday, September 16, 2013

Watu na Ngiri wanaishi kwa karibu ndani ya hifadhi ya Saadani

Saadani National Park, Bagamoyo - Tanzania
Uwepo wa Ngiri wengi hususan kwenye Kijiji cha Saadani ni sifa moja kubwa ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani huko Wilayani Bagamoyo. Ni jambo la kawaida kabisa kuwaona Ngiri (waporini) wakikatisha mitaani sambamba na wakazi wa kijiji hiki. Picha juu ni Mkazi wa Kijiji cha Saadani akielekea kwako huku Ngiri akielekea pembezoni ya barabara kulikwepa gari letu.

 

Saadani National Park, Bagamoyo - Tanzania
Picha ninayoipata hapa ni kama ya mbwa tunaowaona kwenye makazi ya watu. Lakini hapa tunawaona Ngiri. hapa ni ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani, kwenye Kijiji cha Saadani. Hebu fikiria siku moja unaamka asubuhi nyumbani kwako unataka kwenda kwenye shughuli zako, unakutana na Ngiri akiwa mbele ya mlango wa Nyumba yako. Kwa wakazi wa kijiji hiki, hilo ni jambo la kawaida kabisa sambamba na vurugu za Ngedere wanaonyemelea vyakula na wakati mwingine kuingia mpaka ndani ya nyumba.

Saadani National Park, Bagamoyo - Tanzania

Saadani National Park, Bagamoyo - Tanzania
Mbele kidogo walikuwepo hawa Ngiri wengine na Mbuzi wakila pembezoni mwa barabara.

Saadani National Park, Bagamoyo - Tanzania

No comments:

Post a Comment