Thursday, September 19, 2013

Auric Air yazindua Safari za Dar - Njombe kupitia Iringa


Auric Air Tanzania - Njombe
Ni Picha za safari ya uzinduzi wa Ndege za shirika la Auric kati ya Dar Es Salaam na Njombe kupitia Iringa. Picha juu ni ndege ya Auric baada ya kutua kwenye uwanja wa Ndege wa Mkoa Njombe. Kuanzishwa kwa safari hii kutatoa fursa kwa wasafiri wa Mkoa mpya wa Njombe kupata huduma za usafiri wa Anga kati ya mkoa wa Njombe, Iringa na Dar Es Salaam. Shughuli hii ilikuwa ni tarehe 16 Septemba 2013.Auric Air Tanzania - Njombe
Baadhi ya Abiria waliosafiri na ndege hii wakishuka kwenye ndege baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Njombe

Auric Air Tanzania - Njombe
Rubani akijiandaa kuondoka uwanja wa Ndege wa Njombe kurudi Dar kwa kupitia Iringa.

Auric Air Tanzania - Njombe

Auric Air Tanzania - Njombe
Ndege ya Auric Air ikiruka toka kwenye uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Njombe kuendelea na safari zake baada ya safari ya uzinduzi.

Auric Air Tanzania - Njombe
Jengo la Uwanja wa ndege wa Mkoa wa Njombe

Auric Air Tanzania - Njombe

No comments:

Post a Comment