Wengi wetu tumezoea kuona nyayo za wanadamu wenzetu pindi tunapoenda kutembea kwenye fukwe za bahari za mijini na maeneo mengine tunayoishi (yenye fukwe). Kwa Fukwe za bahari ya Hindi ndani ya hifadhi ya Saadani hali ni tofauti na mazoea yetu. huku ukifika pwani, unakutana na nyayo za wanyama ambao walikuwa hapo kabla yako. Jiandae kukuta nyayo ambazo zitakuacha ukishangaa na wakati mwingine baadhi huanza kupatwa na woga. Kwani unaweza ukakuta Nyayo za Sharubu zikiwa zimetapakaa pwani. Siku hii tulikutana na nyayo za Ngedere na baadhi ya Swala waliokuwa wamepita ufukweni hapo. huu ni ufukwe ambao upo karibu kabisa na Geti la Madete.
Moja ya sifa kubwa ya fukwe hii ni kwamba eneo hili ni maarufu sana kwa kuwa na viota vya mayai ya Kasa ambao huogelea Maelfu ya kilometa baharini ili kufika kwenye fukwe hii kwa lengo la kutaga mayai yao. Siku unapokuwa na bahati unapotembelea unaweza ukakutana na kiota ambacho mayai yake yametotoa na hivyo kushuhudia Kasa wadogo wakianza safari yao ya kwanza ya kuogelea. Siku Tulipotembelea hifadhi ya Saadani hakukuwa na kiota ambacho kilikuwa kinaanza kutoa watoto wa Kasa.
Guide tuliyekuwa nae siku hii (Jumanne) akiwa busy kutafuta Nyayo za Sharubu aka Mzee wa pori ambapo alisema mara nyingine huwa zinakuwa zipo maeneo haya. Japo tulikuwa na hamu ya kuziona nyayo hizo lakini naamini kama zingeonekana, basi ni dhahiri kukaa kwetu nje ya gari na kufuarahia mandari ya pwani hii kungesitishwa ghafla na sote tungerudi ndani ya gari tulilokuja nalo hapo bila kujijua.
Hii Pwani ipo Wilaya ya Pangani.
No comments:
Post a Comment