Saturday, September 21, 2013

Ni Ndani ya hifadhi ya Taifa ya Saadani

Ni ndani ya hifadhi ya tiafa ya Saadani tulipokutana na huyu jamaa akitengeneza pikipiki yake iliyoharibika huku mtoto aliyeongozana nae akiwa amesimama pembeni. Alikuwa bize akishughulikia pikipiki yake na hata tuliposimama kujaribu kuona kama kuna msaada wowote wa kutoa, yeye alisema sisi tuendelee kwani tatizo lenyewe kishamaliza kulitatua na baada ya muda mfupi anaendelea na safari yake. hii ilikuwa ni pembezoni mwa barabara inayotoka Bagamoyo kuelekea Tanga ambayo inapita ndani ya hifadhi ya Saadani.


Tulielezwa na guide wetu kuwa hii ni hali ya kawaida na kwa imani za wana  kijiji wa Saadani ni kwamba Simba wa Saadani hawali mtu..... Hii inabaki kuwa imani yao na sio mwongozo wala imani ta Tembea Tanzania. Tahadhari ni muhimu kuchukuliwa uwapo eneo lenye wanyama wakali wa porini.

No comments:

Post a Comment