Saturday, August 3, 2013

Njia ya kuelekea kwenye Kilele cha Mlima Kilimanjaro

Ni Picha moja lakini yenye lengo la kukonyesha kitu kimoja kwa namna tofauti. Mstari mweusi unaoonekana kwenye picha ya juu ndio njia ya kupanda mlima kuelekea kwenye kilele cha Gilmans na Kibo kutokea kituo cha Kibo. Picha hii ilipigwa tukiwa maeneo ya Saddle tukiwa njiani kuelekea kituo cha Kibo tukitokea Horombo. Wengi wetu hupita hii njia usiku wa manane wakati wa kupanda na kurudi asubuhi. Huanza na kuishia kwenye kituo cha Kibo ambacho kwa hapo hakionekani kwani kimefichwa na vilima vingine. Eneo la juu kabisa (ulipoishia mstari) ndio kilipo kituo Gillmans. Baada ya Hapo mpandaji na timu yake watatembea kwa masaa takriban mawili kabla ya kufika Kilele cha Uhuru.

Picha hii nimeondoa mstari ili uweze kuiona njia yenyewe kama ilivyokuwa ikionekana siku hiyo tokea Saddle.

No comments:

Post a Comment