Saturday, May 11, 2013

Waliopanda Mlima Kilimanjaro kwa Njia ya Rongai..

Sio njia zote za kupandia mlima Kilimanjaro ambazo mgeni hushukia pale alipoanzia, Zipo baadhi ambazo mgeni hushukia njia nyingine. Rongai, Umbwe ni njia ambazo zina utaratibu huu. Wa Umbwe hushukia njia ya Mweka wakati wale wa njia ya Rongai hushukia njia ya Marangu. Kwa kuwa Mabanda ya njia ya Marangu ni kwa ajili ya wale wanaoitumia njia ya Marangu, wanaotoka Rongai wao hulala kwenye mahema walioanza nayo safari. Hapa ni kituo cha Mandara na haya mahema ni ya wapandaji wa Mlima Kilimanjaro walioanzia safari yao kwenye geti la Rongai na hapa (Horombo) wakiwa njiani kurudi chini kupitia njia ya Marangu.

Horombo Hut - Marangu route
Hapo kuna mahema ya Kulala (madogo) na kuna mahema ya Mesi (chakula). Wapishi na wagumu wao nao wanalala kwenye mahema yao.

Horombo Hut - Marangu route
Hili lilikuwa kundi jingine likiwa limeshajenga kambi yao.

Horombo Hut - Marangu route
Vifaa vyao vyote hubebwa na Wagumu wao wakiwa safarini.

Horombo Hut - Marangu route
Siku hii Ukungu na baridi vilishika hatamu si mchezo. Sisi tuliokuwa tunalala kwenye mabanda tuliisikia baridi kisawasawa. Sijui hawa ndugu zetu waliolala kwenye haya mahema walikuwa na hali gani usiku mnene ulipotinga. Aina ya malazi unayoyapata ukiwa unapanda mlima Kilimanjaro iwe ni kigezo cha msingi kwenye uchaguzi wa njia ya kupandia Mlima huu.

No comments:

Post a Comment