Sunday, May 5, 2013

Mandhari ya kituo cha Horombo - Marangu route

Horombo Hut, Marangu Route - Mount Kilimanjaro
 Kwa anayepanda mlima Kilimanjaro kwa kupitia njia ya Marangu, Horombo kitakuwa kituo chake cha pili kulala baada ya Mandara. Ni Kituo ambacho wageni (haswa wale wa njia ya Marangu) hulala kwenye mabanda kama ilivyo kwa vituo vingine kwenye njia ya Marangu. Kituo hiki kinatumika pia na wageni waliopanda mlima kutokea njia ya Rongai japo wao hawalali kwenye haya mabanda. Wageni wanaoanzia safari yao kwenye njia ya Rongai hupita Horombo wakiwa wanashuka na mwisho wao huwa ni geti la Marangu. Kuna baadhi ya njia za kupandia mlima ambazo mwisho wa safari huwa ni eneo tofauti na wageni walipoanzia. Rongai na Umbwe zipo ktk mfumo huu.

Horombo Hut, Marangu Route - Mount Kilimanjaro
Unayoyaona ni baadhi ya mabanda ya kulala wageni wanaotumia njia ya Marangu hapa katika kituo cha Horombo. Banda moja linagawanywa katika sehemu mbili huku kila sehemu ikiwa na vitanda vinne. Kwa hiyo banda moja lina uwezo wa kulaza wageni wasiozidi nane (8).

Horombo Hut, Marangu Route - Mount Kilimanjaro
Kitu cheupe unachokiona kwa mbali sio Ziwa au Bwawa bali ni Mawingu. kituo cha Horombo kipo Mita 3720 juu ya usawa wa bahari. unapoyaona mawingu yakionekana kwa chini kiasi hiki unaweza kupta picha ya kuwa mtu aliyeopo Horombo yupo juu kiasi gani tokea usawa wa bahari.

Horombo Hut, Marangu Route - Mount Kilimanjaro
Hii ni view tuliyokuwa tukiipata tokea kwenye hut yetu. Banda letu lilikuwa ni moja ya mabanda yaliyojengwa enero la nyuma la kituo cha Horombo ambako kulikuwa na korongo na mto unaopita kwenye korongo hilo. Mimeo inayoota huku juu ni tofauti na ile tuliyoiona Mandara na maeneo mengine ya chini.

Horombo Hut, Marangu Route - Mount Kilimanjaro
Kijua cha asubuhi.

Horombo Hut, Marangu Route - Mount Kilimanjaro

Horombo Hut, Marangu Route - Mount Kilimanjaro
Kilele cha Mawenzi kikionekana kwa nyuma ya Kituo cha Horombo.

Horombo Hut, Marangu Route - Mount Kilimanjaro
Kibao cha kukukaribisha Horombo, Mabanda ya kulala wasaidizi na wasindikizaji wageni. Kilele cha Kibo kikionekana kwa chati kwa nyuma

Horombo Hut, Marangu Route - Mount Kilimanjaro
Asubuhi moja kwenye kituo cha Horombo, Mabanda yanayoonekana zaidi hutumiwa na wabeba mizigo pamoja na maguide wanapofika horombo. Unaowaona kushoto ni 'wagumu' wakiwa bize kuandaa kifungua kinywa kwa ajili ya wageni wao. Huko wanapotokea ndio kuna majiko.

Horombo Hut, Marangu Route - Mount Kilimanjaro
Sio kawaida kwa kilele cha Mawenzi kuwa na barafu lakini hali ya baridi na mvua vikizidi, kilele hiki hupata barafu kwa namna. Safari hii barafu ilikuwa ya kutosha na ilikuwa inaonekana bila wasiwasi. Kipindi cha joto na kiangazi, Kilele hiki hubakia kuwa kama jabali la mawe. Hakuna nayeruhusiwa kupanda kwenye kilele hiki kutokana na hatari ya mawe yanayoporomoka. Kilele cha Kibo ndio kinatumika na watalii.

No comments:

Post a Comment