Saturday, May 4, 2013

Banda tulipolala kwenye Kituo cha Horombo - Marangu routePicha juu ni Banda ambalo tulilala kwenye kituo cha Horombo wakati wa kupanda na wakati wa kushuka. kwenye mpango wetu wa safari ya kupanda mlima tulipanga kukaa Horombo siku mbili kufanya aclamatization na pia kulala hapo usiku mmoja wakati tukitokea Kibo kurudi uraiani. Mara zote hizi tulilala hapa. Si lazima mgeni kulala hapo hapo lakini wakati tukishuka tuliomba tulale banda tulilolizoea, kwa bahati nzuri hakukuwa na wengine waliopangwa kulala humo siku hii. Tulipangiwa upande wa nyumba ambao ulikuwa kama unaangaliana na kilele cha Mawenzi.

Mbele ya banda letu kulikuwa na mteremko mkali ambao ulikuwa ukielekea kwenye mto unaopita nyuma na pembezoni ya kituo cha Horombo.

No comments:

Post a Comment