Saturday, April 13, 2013

Vifaa muhimu vya mpandaji vinapatikana getini Marangu kwa kukodisha

Marangu Gate, Mount Kilimanjaro - Tanzania
Kontena mbele lipo ndani ya eneo la Marangu gate ni kwa ajili ya kukodishia vifaa mbalimbali ambavyo mpandaji analazimika kuwa navyo kwa safari ya kwenda Kilele cha Uhuru. Hapa utapata mavazi muhimu kama makoti ya baridi na yale ya mvua, mifuko ya kulalia (sleeping bags) sambamba na viatu maalumu kwa kutembelea kwenye barafu na baridi kali. Hii hutumiwa na wapandaji ambao hatuna vifaa hivi (kutokana na mazingira tunayoishi kila siku) au kwa wageni ambao hawapendi kubeba na kusafiri na mizigo mingi - hususan wageni wanaokuja ndege kwa ndege, usafiri ambao kila kilo inahesabiwa na kumgharimu msafiri endapo atazidisha kiwango alichowekewa. Baadhi ya vifaa ni vizito na vingine vinachukua ujazo mkubwa.

Marangu Gate, Mount Kilimanjaro - Tanzania
Mimi (kulia) na Mdau Frank T tukiendelea kujaribisha vifaa mbalimbali ambavyo tulikodisha hapo getini.

Marangu Gate, Mount Kilimanjaro - Tanzania
 Layer upon layer, zana zinazidi kuongezeka. Hapa nikijaribu nguo za Mvua ambazo huwa za mwisho kuvaliwa baada ya kuvaa nyingine zote. Majaribio haya ni muhimu kwani unaweza ukachagua kitu kwa kuangalia kwa macho halafu kisijekukutosha mbele ya safari au kuwa na dosari yoyote na kukuweka kwenye hatari. Wasindikizaji huwa wanatoa msaada wa vifaa gani uchukue na ni wakati gani unahitajika kuvaa nini kutegemea hali ya hewa na urefu tokea juu ya usawa wa bahari. Mfuko uliochini ndio ulibeba sehemu kubwa ya hivi vifaa na mfuko huo ulikuwa unabebwa na porters. Mabegi yetu ya mgongoni yalikuwa zaidi kwa kubebea vitu kama Camera, Maji na vitu vidogo vidogo vya binafsi.

Marangu Gate, Mount Kilimanjaro - Tanzania
Baada ya kutupia gloves; Frank akiendelea kuchagua koti la Mvua. Mwishowe alichukua alilokuwa akijaribisha hapo.

Marangu Gate, Mount Kilimanjaro - Tanzania

No comments:

Post a Comment