Tuesday, April 30, 2013

Polepole ndio mwendo wake

Tarangire National park
Ukiachia wanyama wakubwa tuliozoea kuwaona, hifadhi zetu hapa nchini zina wanyama wadogo ambao inawezekana wasiwepo kwenye list ya wanyama ambao mgeni anapenda kuwaona lakini wanapoonekana huwa ni tukio la simulizi pia. Uwepo wao ni sababu nyingine ya dereva kuwa makini awapo ndani ya eneo la hifadhi. Mwendo kasi na umakini ni umuhimu unapokuwa ndani ya hifadhi au pori la akiba. picha juu ni Kobe ambae mdau Thomas wa HSK safaris alikutana nae hivi karibuni ndani ya hifadhi ya Taifa ya Tarangire. 

No comments:

Post a Comment