Tuesday, March 5, 2013

Kili Marathon ya mwaka huu ilivuta wengi

Yaelezwa ya kwamba washirikia zaidi ya 7000 wameshirikia mwaka huu katika mashindano ya ngazi tofauti. Mwaka huu kulikuwa na 5 Km Fun run, Half Marathon (21km) na Full Marathon (42Km). Kila mmoja alipata fursa ya kuchagua mashindano yanayoendana na maandalizi yake. Mdau John Kesy wa Moshi yeye alishirikia Half Marathon na ndiye aliyetutumia picha hizi.

Washiriki wakiendelea kuchanja mbuga kwenye mitaa mbalimbali ya jiji la Moshi na meneo karibu yake.

Mlima Kilimanjaro ukionekana vyema kwa nyuma huku wakiendelea na kutimua mbio


Kituo kimojawapo cha kugawia maji kwa wakimbiaji kilichowekwa mitaa ya Mweka. 

Kwa wale ambao hawakushiriki mbio zozote, kulikuwa na burudani mbalimbali kuwaburudisha wakati wengine wakiendelea na mbio. Shukran ya picha kwa mdau John Kessy wa Moshi.

No comments:

Post a Comment