Saturday, February 9, 2013

Taswira za kutoka Serengeti Mchana huu

Ni Picha ambazo mdau Thomas wa HSK Safaris (katikati) amezipiga na kunitumia leo hii akiwa maeneo ya Ndutu, ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Kwa mujibu wa mazungumzo yangu naye amenieleza ya kwamba sasa hivi Nyumbu wengi wapo maeneo hayo hali inayopelekea wageni wengi kufurika maeneo ya Ndutu kuwaona mamia na maelfu ya Wahamaji. Eneo la Ndutu lipo kusini magharibi mwa hifadhi ya taifa ya Serengeti na ndio huko inakopatikana pia hoteli ya Ndutu.

Ujio wa wahamaji ni neema na fursa ya msosi kwa wakazi wengine wa hifadhi hii. Mida ya mchana pia Mdau Thomas na wageni wake walibahatika kuwaona Duma aka wa chini wawili wakiwa wamepumzika chini ya mti. Kwa mbali nyuma utaweza kuona moja ya makundi ya nyumbu wanaohama likitimua vumbi.
Kama nawe unapicha ya porini iwe ya leo leo au hata ya siku nyingi tutumie kupitia tembeatz@gmail.com nasi tutaipa nafasihapa kwenye blog ya utalii ya Tembea Tanzania mara moja
Shukran ya picha hizi kwa mdau Thomas wa HSK Safaris.

No comments:

Post a Comment